Pages

lundi 20 octobre 2014

WANANCBHI WA BENI HAWANA IMANI NA VIONGOZI WAO BAADA YA KUTOKEA MAUAJI

wananchi wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo DRC, hawanaimani na kauli za viongozi wa eneo hilo baada ya kutokea kwa mauaji ya raia wasiokuwa na hatia, chini ya mkono wa kundi la waasi wa Uganda wa ADF-Nalu.
Licha ya wito uliotolewa na mea wa jiji la Beni Nyoni Masumbuko kuwataka kusalia kuwa watulivu katika kipindi hiki jeshi la serikali likifuatilia kwa ukaribu zaidi swala la Usalama, wananchi wengi wameendelea kuutoroka mji huo.

Kundi la ADF-Nalu limeendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia yoyote licha ya jeshi la serikali kutangaza kuwa limewadhibiti kwa asilimia kubwa waasi hao.

Wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakihoji kuhusu uwezo wa kundi hilo kuingia hadi katika eneo ambalo linawakaazi wengi wakiwemo wanajeshi wa serikali na kutekeleza mauaji kwa kuwakata watu kwa mapanga na kufaulu kutoroka bila wasiwasi yoyote.

Hayo yanajiri wakati huu wafungwa katika jela la Butemba masharik wa DRCongo wakifaulu kutoroka, na kuzua mtafaruku mkubwa katika eneo hilo.

mardi 7 octobre 2014

KUNDI LILILO ASI CHAMA CHA FNL LAKIRI KUHUSIKA KATIKA SHAMBULIO LA JESHI LA BURUNDI


Kundi moja la waasi nchini Burundi, limejigamba hapo jana kuhusika katika shambulio dhidi ya kituo kimoja cha kijeshi nchini humo karibu na mpaka na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na kukiri kuwauwa wanajeshi sita katika shambulio hilo, idadi iliokanushwa na jeshi la taifa hilo.

Msejaji wa jeshi la Burundi kanali Gaspard Baratuza amefahamisha kwamba kulikuwa na makabiliano na kundi la wahuni, na kukanusha taarifa ya kupoteza wanajeshi, badala yake kuthibitisha kuwa wamemuua muasi mmoja katika shambulio hilo.

Kundi hilo la waasi linasadikiwa kuwa ni miongoni mwa wafuasi wa chama cha FNL walioasi na kuanzisha uasi. Kulingana na msemaji wa kundi hilo Felix Jean Ntahonguriye amethibitisha kwamba walishambulia kituo cha jeshi kilichopo katika tarafa ya Gihanga kwenye umbali wa kilometa zaidi ya Ishirini na jiji la Bujumbura na baadae kutokomea katika msitu wa Rukoko karibu na DRCongo.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kundi hilo limekuwa likijigamba kuhusika na mashambulizi kadhaa ambapo kulingana na msemaji wa kundi hilo wataendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya vituo vya jeshi la Burundi hadi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.


msemaji wa jeshi la Burundi Gaspard Baratuza amepuuzia kitisho hicho na kusema kwamba ni kundi la wahuni waliopoteza dira na haliwezi kupambana na jeshi la serikali.

HERVE LADSOUS KUHUDHIRIA SHEREHE ZA KUAGWA KWA MIILI YA WANAJESHI WA UN JIJINI BAMAKO


Herve Ladsous naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anaye husika na opersheni za kulinda amani yupo nchini Mali ambako atahudhuria sherehe za kuiaga miili ya wanajeshi tisa wa Nigeria waliouawa katika shambulio liliotokea siku ya Ijuma juma lililopita.

Miili ya wanajeshi hao tisa wa kulinda amani kutoka nchini Nigeria itawekwa nje kwenye makao makuu ya vikosi vya kulinda amani jijini Bamako ambako mawaziri Abdoulaye Diop, wa mambo ya ndani nchini Mali pamoja na waziri wa Ulinzi Meja Kanali Bah Ndaw wanatahudhiria

Upande wa Minsuma, mbali na Herve Ladsous atakuwepo pia Arnaud Acodjénou naibu kiongozi wa opersheni za Umoja wa Mataifa, ambao wamekuja kutowa heshima za mwishi kwa wanajeshi hao waliojitolea kwa ajili ya amani barani Afrika. Herve Ladsous atatumia fursa hiyo kukutana na rais wa Mali Ibrahima Bubakar keita.


Herve Ladsous atajadili pia kuhusu swala la wanajeshi wa kulinda amani kutoka nchini Tchad ambao wanatishio kurejea nyumbani baada ya kupoteza mara kadhaa wanajeshi wake kutokana na bomu za kutegwa ardhini zilizo tengwa na wanamgambo.

WAZIRI WA ULINZI WA ZAMANI AIKOSOA SERA YA OBAMA KUOPAMBANA NA ISLAMIC STATE


Waziri wa zamani wa ulinzi wa serikali ya Marekani Leon Paneta na kiongozi wa zamani wa idara ya ujasusi, ambaye kitabu chake Worthy Fights kinazinduliwa hii leo, ameikosoa sera ya rais Obama kupambana na Ugaidi nchini Iraq na Syria, na kuonya kwamba kwa hali ilivyo vita hivyo vinaweza kudumu miaka 30.


wakati vita dhidi ya kundi la IS ikipamba moto, huku wanajihadi wa hao wakiendelea kumudu kwenye uwanja wa mapambano dhidi ya mashambulizi ya majeshi ya muungano, waziir wa ulinzi wa zamani amejitokeza na kuvunja ukimya kwa kutowa kauli ambayo imeighadhabisha Ikulu ya Marekani ya White House.

lundi 6 octobre 2014

MPIGA PICHA RAIA WA MAREKANI AREJESHWA NYUMBANI BAADA YA KUAMBUKIWA NA EBOLA LIBERIA


Mpiga picha raia wa marekani aliepata mambukizi ya virus vya Ebola nchini Liberia amesafirishwa kuondoka jijini Monrovia, duru za mashirika ya kibinadamu zimearifu.

Ashoka Mukpo mwenye umri wa miaka 33 mpiga picha na ambaye aliajiriwa hivi karibuni na kituo cha Marekani cha NBC aliwekwa katika hali ya hatari tangu jumatano juma lililopita katika kituo cha shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka.


Mwenyekiti wa kituo cha NBC Deborah Turness alifahamisha tangu siku ya Ijumaa iliopita kwamba mpiga picha huyo atasafirishwa hadi kwenye kituo kingine kwa ajili ya matibabu zaidi, huku wengine ambao hawaonyeshi dalili zozote za virusi vya Ebola watarejeshwa nyumbani na kuwekwa kqenye hali ya hatari kwa kipindi cha siku 21 kama inavtogizwa.

KUNDI LA MUJAO LAJIGAMBA KUHUSIKA KATIKA SHMBULIO LA VIKOSI VYA UN


Mpiganaji mmoja wa kijihadi wa kundi la Mujao, moja miongoni mwa makundi yalio kalia eneo la kaskazini mwa Mali amejigamba kuhusika na shambulio la kujitowa muhanga dhidi ya Kikosi cha Umoja wa mataifa nchini Humo.

Shambulio la siku ya Ijumaa dhidi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha majeshi kutoka nchini nigeria lilisababisha vifo vya watu 9.

Uongozi wa kikosi cha Kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Minusma, umesema hili ni shambulio kubwa kuwahi kutokea tangu kutumwa kwa majeshi ya Umoja wa Mataifa tangu kutumwa kwake Julay 2013.


AL SHABAB WAPOTEZA NGOME YAO MUHIMU


Askari wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na jeshi la Somalia wamefanikiwa siku ya Jumapili kuuteka mji wa Barawe, ngome ya mwisho ya wanamgambo wa Al-Shebab na bandari kuu ambayo ilikuwa bado iko mikononi mwao.


Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa hatua hii ni pigo kwa wanamgambo wa Al-Shabab ambao walikuwa wanatumia bandari hii kupitisha chakula, kuuza mkaa pamoja na kupokea wapiganaji wake wa kigeni wanaoingia nchini humo.


Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa hatua hii ni pigo kwa wanamgambo wa Al-Shabab ambao walikuwa wanatumia bandari hii kupitisha chakula, kuuza mkaa pamoja na kupokea wapiganaji wake wa kigeni wanaoingia nchini humo.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...