Pages

vendredi 22 juillet 2016

TANZANIA YAZUIA USAFIRISHAJI WA CHAKULA KUELEKEA NJE YA NCHI


Tanzania imezuia usafirishaji wa mazao ya vyakula nje ya nchi natayari madhara yake yameanza kushuhudiwa ndani na nje ya nchi.


Rusumo, Kabanga na Kobero kwenye mipaka baina ya Tanzania,Rwanda na Burundi kumeshuhudiwa utekelezwaji wa amri ya serikali ya Tanzania kutosafirisha mazao nje ya nchi. Bw Thabiti Chiwalo ni afisa afya ya mimea na mazao mpakani Kabanga amesema kwamba wamepokea taarifa kupitia idara ya ukaguzi wa mazoa kwamba mazao ya aina yoyote yasipite mpakani na zoezi hilo litandelea hadi pale utaratibu utapo badilika.


Kwa sasa hakuna huduma yoyote ya kutoa mazao yoyote kutoka Tanzania kuelekea Burundi. Thabiti amebainisha kuwa madhara ya usafirishaji mazao yameonekana zaidi kwenye mpaka wa Rusumo, anasema hali ni mbaya zaidi katika mpaka huo ambapo kuna malori zaidi ya 50 ambapo nafaka za chakula kama maharage, mahindi, mchele, kutoka na hatuwa hiyo inabidi malori hayo yarejea nchini Tanzania.


Hatuwa hiyo ya Tanzania, imesababisha ugumu wa maisha kwa wananchi wa Burundi hususan wa maeneoya mpakani ambao wanasema wameshuudiwa malori ya mizigo yakigeuza kurudu Tanzania kama ilivyo elekezwa na serikali.


Licha ya Tanzania kupiga marufuku usafirishaji wa mazao nje ya nchi na baadhi ya maafisa kusimamishwa kazi kwa kutoa vibali vya kusafirisha mazao nje, lengo kuu ikiwa ni kuhakiki akiba ya chakula nchini, baadhi ya maafisa wameiambia RFI kuwa mazao hayo yanasafirishwa kupitia njiazisizo halali. Julian Rubavu RFI.


lundi 18 juillet 2016

RAIS WA UTURUKI AAHIDI KUMALIZA KILE ALICHOKIITA VIRUSI

Mamlaka nchini Uturuki zimeendelea na operesheni ya kuwasaka na kuwakamata watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi lililoshindikana, dhidi ya Rais Racep Tayyip Erdogan, ambapo mpaka sasa watu zaidi ya elfu 6 wanashikiliwa, huku Serikali ikiapa kumaliza kile ilichokiita “Virusi”.

Hapo jana wakati rais Erdogan akihudhuria ibada maalumu ya mazishi kuwakumbuka raia na wanajeshi waliouawa wakati wa jaribio la mapinduzi, amesema kuwa nchi yake inafikiria upya kurejesha adhabu ya kifo, licha ya wasiwasi ulioneshwa na jumuiya ya Kimataifa.

Viongozi wa dunia, akiwemo Rais wa Marekani, Barack Obama, wamealaani jaribio la mapinduzi lililoshindikana Ijumaa ya wiki iliyopita na wanajeshi walioasi, ambapo kwa mujibu wa Serikali watu zaidi ya 300 waliuawa.

Hata hivyo kumekuwa na hofu ya kutekelezwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa watuhumiwa wa jaribio hilo, baada ya kuonekana kwa picha zikiwaonesha maofisa wa Serikali wakiwanyanyasa wanaodaiwa kuwa ni watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi.

Waziri wa sheria wa Uturuki, Bekir Bozdag, amesema kuwa watu wanaokadiriwa kufikia elfu 6 wamekamatwa katika operesheni maalumu ya kusafisha jeshi na taasisi za Serekali ambazo anadai zimevamiwa na watu wanaotaka kutekeleza mapinduzi, huku akionya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.


PADRI MALU MALU KUZIKWA LEO MJINI BUTEMBO

Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI, padre Apolinaire Malu Malu Muholongu, umewasili katika mji wa Butembo mkoani Kivu ya kaskazini ambako unatarajiwa kuzikwa hivi leo.

Kabla ya kusafirishwa hadi Butembo, mwili wa kiongozi huyo uliagwa na umati wa watu mjini Kinshasa, wakiwemo wanasiasa na maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC.


Katika kuithamini kazi yake na juhudi nyingi za kidiplomasia alizoongoza kwa niaba ya serikali ya nchi hiyo, Rais Joseph Kabila, amemtaja Malumalu kama shujaa, akifananisha yale aliyoyafanya na viongozi maarufu nchini humo kama, Emery Patrice Lumumba na marehemu Laurent Desire Kabila.

AU WAJADILI USALAMA WA SUDANI KUSINI NA BURUNDI

Viongozi wa Umoja wa Afrika wanajdili kuhusu usalama wa Sudani Kusini na Burundi ambako mzozo wa kisiasa umeendelea kutokota katika nchi hizo, na ambapo mwenyekiti wa Umoja huo amewatolea wito viongozi wa mataifa hayo kuheshemu makubaliano na mikataba mbalimbali iliofikiwa.

wakati huo huo rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na makamu wake wa kwanza wa Rais Riek Machar, wamekubali kukutana kwa mazungumzo, ili kusaka muafaka wa kurejesha amani nchini humo, baada ya mapigano yaliyoshuhudiwa juma moja lililopita.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume inayosimamia utekelezwaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini na viongozi hao kumaliza vita nchini humo, Festus Mogae, amethibitisha Rais Kiir kuzungumza kwa njia ya simu na Riek Machar na kukubaliana kukutana, wakati huu pia jumuiya ya nchi za IGAD, ikifikiria kutuma wanajeshi elfu 14 nchini Sudan Kusini kulinda amani.

Viongozi Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika, wanaotarajiwa kutamatisha kikao chao hivi leo jijini Kigali, Rwanda, wanatarajiwa kutoka na maazimio kuhusu kinachoshuhudiwa kwenye nchi hiyo.

Hata hivyo maswali bado ni mengi ikiwa kweli wakuu hawa wa nchi wana nia ya dhati ya kumaliza machafuko Sudan Kusini, na kama watatoka na maazimio mahsusi kumaliza mgogoro wa nchi hiyo.


Haji Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa, akiwa jijini Dar es Salaam, Tanzania na hapa anaeleza mtazamo wake.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...