Rais
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John pombe Magufuli, hii leo kwa
mara ya kwanza amelihutubia bunge huku akiahidi kuwa serikali yake
itafanya kazi kwa weledi, wakati huu pia akimwapisha waziri mkuu
mpya, Majaliwa Kassim Majaliwa.
Ni
sauti yake waziri mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa,
wakati akila kiapo hii leo mjini dodoma katika ikulu ndogo ya
Chamwino, sherehe ambayo mbali na kuhudhiriwa na rais wa Zanzibar na
viongozi wastaafu, wabunge na wageni mbalimbali nao walihudhuria.
Baada
ya sherehe za kuapishwa kwa waziri mkuu, baadae wabunge walirejea
bungeni ambako rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Pombe
Magufuli aliwahutubia, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo
toka alipoteuliwa kuwa rais baada ya uchaguzi wa October 25 mwaka
huu.
Kwenye
hotuba yake rais Magufuli, aliwashukuru wananchi kwa mara nyingine
kwa kumuamini na kumchagua, ambapo ameahidi kuwa kiongozi
atakayewatumikia watu wote bila kubagua, na kwamba lengo lake ni
kuhakikisha nchi ya tanzania inasonga mebel kimaendeleo.
Rais
Magufuli pia kwenye hotuba yake pia akaeleza malalamiko aliyoyapokea
kwa wananchi ambayo yeye anaona ni kero kwa wananchi, maeneo ambayo
anasema ni lazima yashughulikiwe ipasavyo ili kuleta uaminifu kwa
wananchi.
Kuhusu
Uchumi rais Magufuli amesema kuwa serikali yake itakuwa ni serikali
ya viwanda itakayosimamia sheria na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi
unasimama kwa kujenga na kuendelea viwanda ili kutengeneza ajira
zaidi.
katika
hotuba yake pia, rais magufuli hakuacha kugusia suala la katiba mpya,
ambapo amesema atahakikisha serikali yake inasimamia mchakato huo na
kwamba safari hii utakamilika kwa wakati.
Rais
Magufuli pia akagusia suala la muungano pamoja na hali ya kisiasa
visiwani zanzibar ambapo amesema yeye ni muumini mkubwa wa muungano
uliopo na kwamba anaamini mgogoro wa zanzibar uliojtokeza unatatuliwa
kwa amani.
Kabla
ya kuanza kwa hotuba yake bungeni, rais Magufuli alishuhudia vioja
vya upinzani ambao walikuwa wakipiga kelele wakati viongozi wa
zanzibar walipokuwa wakiingia bungeni bungeni, ambapo baadae spika wa
bunge Job Ndugai alilazimika kutumia kiti chake kuwafukuza nje ya
ukumbi wa bunge ili kupisha hotuba ya rais kuanza, jambo ambalo
upinzani ulitii na kutoka nje.