Pages

mardi 31 mars 2015

AGATHON RWASA AITAKA CENI KUONGEZA MUDA WA WAGOMBEA UCHAGUZI KUWASILISHA FAILI ZAO

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi wa chama cha FNL tawi lisilo tambulika na serikali Agathon Rwasa ametowa wito kwa tume ya uchaguzi nchini humo kuongeza muda wa zaidi kwa wagombea kuwasilisha faili zao, wakati huu tume ya uchaguzi CENI ikianza kupokea faili za wagombea katika chaguzi mbalimbali.

Agathon Rwasa amesema kutokana na muda wa majuma mawili na idadi ya wagombea, muda uliotolewa hautotosha, hivyo unahitajika muda zaidi. Rwasa ametuhumu pia baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiwazuia kuwafikia wafuasi wao na hata kuwahutubia.

MAKAM MWENYEKITI WA SAHWANYA FRODEBU ASEMA MAANDAMANO YA AMANI YAGEUZWA KUWA KAMPENI ZA CHAMA TAWALA

Makam wa rais wa zamani nchini Burundi Frederick Banvuginyumvira ambae pia ni naibu mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Sahwanya Fredebu, amesema maandamano ya amani yanayoandaliwa na waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana ni kampeni tosha za kisasa za chama cha CNDD-FDD.

Banvuginyuvira amesema waandamanaji wanaondamana kwa ajili ya amani hawawezi kuimba na kutowa wito wa kumchaguwa Nkurunziza huku wakionyesha picha yake pamoja na ujumbe wanaotowa wa vitisho dhidi ya wanasiasa wa upinzani na wanaharakati wa mashrika ya kiraia.

Makam huyo wa rais wa zamani ameitaka tume ya uchaguzi kutoendelea kukaa kimya kiasi cha kuonekana kwamba inaunga mkono hali hiyo, amewataka pia viongozi wakuu wa serikali kutafuta suluhu ya matatizo ya warundi na sio kuendelea kuwatumia wananchi.

lundi 30 mars 2015

MKANGANYIKO WAENDELEA KUSHUHUDIWA KATIKA CHAMA TAWALA NCHINI BURUNDI

Wakati shinikizo likiendelea kutolewa kutoka ndani na nje ya Burundi kumtaka rais Pierre Nkurunziza kutowania uchaguzi mkuu wa Juni mwaka huu nchini humo, rais Nkurunziza amewafuta kazi wajumbe wa chama tawala cha CNDD-FDD waliosaini waraka wa kumtaka kutowania muhula mwingine wa 3.

Gervais Abayeho aliekuwa naibu msemaji wa rais amechukuwa nafasi ya Leonidas Hatungimana aliekuwa msemaji wa rais kabla kuonyesha msimamo wake dhidi ya muhula wa tatu wa rais Nkurunziza.

Jerome Nzokirantevye aliekuwa msemaji wa Baraza la Seneti ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa Radio na Televishieni ya taifa kuchukuwa nafasi ya Tadee Siryumunsi ambae ni miongoni mwa vigogo wa chama tawala wanaopinga muhula wa 3 wa rais Nkurunziza.

HUYU HAPA NDIE RAIA WA BURUNDI ALIEKAMATWA KWA KUSHUKIWA KUWA AL SHABAB KUTOKANA NA NDEVU ZAKE

Anaitwa Bigirimana, anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 31, raia wa Burundi anaeshi Uganda, hapo jana alitiwa nguvuni baada ya kushukiwa kuwa mfuasi wa Al Shabab. hii imetokana na ndevu zake. jambo ambalo limeibuwa mjadala iwapo kila anaefuga ndevu kiasi hicho ni muislam.

Bigirimana alikamatwa akiwa kanisa wakati wa Ibada ya Jumapili ya Matende( Dimanche de rameaux) baada ya waumini kumshku na kutowa ripoti kwa polisi. baada ya uchunguzi, aliachiwa huru  baada ya polisi wa Uganda kujiridhisha kwamba sio mfuasi wa Al Shabab na kwamba ni muumini wa dini katoliki.

Juma lililopita Marekani ilifahamisha kwamba kundi la Al shabab limepanga kufanya mashambulizi ya kujitowa muhanga kwa mara nyingine tena nchini Uganda baada ya lile lilifanyika mwaka 2010 lililogharimu maisha ya watu zaidi ya 70.


lundi 16 mars 2015

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI BURUNDI AGATHON RWASA AVITUHUMU VYOMBO VYA USALAMA KUHUSIKA NA JARIBIO LA MAUAJI YA MKEWE


Hali ya afya ya mke wa kiongozi wa upinzani nchini burundi Agathon Rwasa yaelezwa kuimarika baada ya kushambuliwa hapo jana Jumapili wakati akiwa kwenye saloon ya kutengeneza Nywele.

Tukio hilo liliotokea katika kata ya warabuni jijini Bujumbura wakati bi Annonciate Haberisoni alipokuwa akitengeneza nywele ambapo mtu aliekuwa na bastola aliingia saloon na kumfyatulia risase kichwani, lakini kwa bahati nzuri mfanyakazi wa Saloon alimsukuma na hivo kunusurika kimiujiza na kumjeruhi kichwani.

Agathon Rwansa anasema kwa sasa mkwe anaendelea vizuri, na muda wowote atarhusiwa kurejea nyumbani huku akivitumu vyombo vya usalama kuhusika na tukio hilo.

Aidha Kiongozi huyo wa tawi la chama cha FNL lisilo tambulika serikalini licha ya kuw ana ushawishi mkubwa, amemtaka rais Nkurunziza kutoingilia familia yake na kwamba iwapo anamatitizo na kiongozi huyo mkewe au mwanae hana tatizo lolote.


Mbali na hayo Agathon Rwasa ametaja majina kadhaa ya watu waliorodheshwa kuuawa katika kipindi hiki kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, katika orodha amabayo amesema imepangwa na viongozi wa idara ya Usalama.

Tukio hilo limetokea wakati huu joto la kisisa likiendelea kupanda nchini humo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais wa Juni utaofanyika baada ya ule wa Bunge na seneti mwezi Mei

mardi 10 mars 2015

SIMONE GBAGBO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 20 JELA

Simone Gbagbo mke wa rais wa zamani wa cote di'Ivoire Larent Gbagbo amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kutokana na makosa yaliotendeka baada ya uchaguzi wa mwaka 2010-2011.


Jopo la majaji wote kwa pamoja wamemuhukumu Simone Gbagbo kifungo cha miaka 20 kutokana na ushiriki wake katika harakati za vurugu na kuyumbisha usalama wa taifa.


Taarifa hii imetolewa na jaji mkuu Tahirou Dembele baada ya jopo hilo la majaji kukutana kwa muda wa saa tisa. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa tangu desemba mwaka jana.

SERIKALI YA BURUNDI YAPUUZIA WITO WA HUSSEIN RADJABU KINARA ZAMANI WA CHAMA TAWALA CHA CNDD-FDD

Hussein Radjabu mwenyekiti zamani wa chama tawala cha CNDD-FDD















Baada ya mwenyekiti zamani wa chama tawala nchini Burundi Hussein Radjabu kujitokeza kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa ikiwa ni majuma kadhaa baada ya kuwepo kwa taarifa za kutoroka jela na kutowa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kutovumilia uvunjifu wa sheria ya Burundi kwa kumruhusu Nkurunziza kuwania uchaguzi kwa muhula wa 3, serikali imesema Hussein Radjabu ni mtu anaependa uasi, hivyo hana nafasi kwa sasa nchini Burundi.

Hussein Radjabu Mwenyekiti zamani wa chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kuwepo na taarifa za kutoroka kwake katika jela kuu la Mpimba jijini Bujumbura.

Akihojiwa na idhaa mbalimbali za kimataifa, Hussein Radjabu amesema Kwa sasa yupo katika eneo salama, pamoja na wananchi.

Katika mahojiano hayo, Hussein Rajabu amesema hakutoroka jela kama inavyoelzwa huku na kule bali kilichotokea faili lake lilikuwa tayari, lakini rais Nkurunziza alikuwa bado amebana kwa sababu azijuazo mwenyewe, lakini kutokana na watu wa karibu waliokuwa pamoja katika harakati za kuwania demokrasia, hawakupenda kuona naendelea kueshi katika jela katika kipindi hiki ambacho kulikuw ana mpango wa kuendesha vurugu katika jela ili wamzuri.

Akieleza namna alivyoondoka katika jela kuu ka mpimba, kinara huyo zamani wa CNDD-FDD amesema aliondoka kwa heshima na tahadhwima hadi eneo alipo kwa wakati huu.

Akizungumzia kuhusu hali ya siasa nchini mwake na iwapo ana nia ya kurejea nyumbani kushiriki kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi June mwaka huu, mwenyekiti huyo wa zamani wa CNDD-FDD amesema tatizo lililopo sio ushiriki wake au la bali ni utawala uliopo hautaki kuheshimu misingi ya demokrasia.

Willy Nyamitwe msemaji wa rais Nkurunziza
Aidha, kongozi huyo ametowa wito kwa raia na wanasiasa wa Burundi kushikamana ili kuboresha hali ya kisiasa iliopo nchini Burundi ambapo amesema hakuna kinachoendeka, kila kitu kipo katika hali ya sintofaham, hususan maandalizi ya uchaguzi.
Upande wake serikali ya Burundi imesema Radjabu bado hajamaliza kutumikia kifungo chake na kwa vile ni mtu hatari ambaye anaweza kutishia amani nchini Burundi, serikali inajipanga kukabiliana na hali yoyote hiyo kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali tulivu.
Msemaji wa rais Nkurunziza kupitia radio ya dunia RFI mapema leo asubuhi amesema Radjabu ni mtu anaefahamika kuwa na tabia ya kuunda makundi ya uasi, hivyo katika kipindi hiki hana nafasi.



lundi 9 mars 2015

MTOTO MWINGINE ALBINO AKATWA KIGANJA CHA MKONO


wakati kampeni ya kupiga vita mauaji ya watu wenye umelavu ikiendelea nchini Tanzania, polisi nchini humoe imsesma hapo jana kwamba mtoto mmoja mwenye ulemavu wa ngozi amekatwa Kiganja cha mkono wake wa kushoto na kundi la watu wasiojulikana.

Baraka Cosmos mtoto mwenye ulemavu wa ngozi alikuwa amelala na mama yake katika kijiji cha Kipenda kusini magharibi mwa Mkoa wa Rukwa ambapo kundi la majambazi waliingia na kumteka mtoto huoyo kabla ya kumjeruhi mama yake.

Duru za polisi zinaeleza kwamba majambazi hao walimpiga mama wa mtoto huyo Prisca Shabani baada ya kukataa kuwapa mwanae na ambapo walitumia panga kwa kukata kiganja cha mkono wa kushoto wa mtoto huyo ambae baadae alipelekwa Hospitalini na mama yake.

Juma lililopita mahakama kaskazini mashariki mwa Tanzania iliwahukumu kunyongwa watu wanne kwa kuhusika na mauji ya mwanamama mmoja mlemavu wa ngozi.

Tukio hili linatokea wakati huu nchini Tanzania kukwa na kampeni kambambe ya kupiga vita mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozo (Albino)

hii ni ishara kwamba kampeni hiyo imefeli, na watu waache kuuza sura kwenye mitandao ya kijamii kwa kuendesha shughuli zisizokuwa na matunda mazuri.

vendredi 6 mars 2015

UMOJA WA ULAYA WAONYA KUHUSU MUHULA WA 3 WA RAIS NKURUNZIZA

Umoja wa Ulaya kupitia muakilishi wake jijini Bujumbura Patrick Spirlet ameonya kuhusu muhula wa 3 wa rais Nkurunziza katika uchaguzi mkuu wa Rais wa Juni nchini humo kwamba unaweza kuzua machafuko katika nchi hiyo.


Joto la kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais nchini Burundi limeanza kupanda wakati huu kukiwa na shaka kwamba rais Nkurunziza anampango wa kuwania muhula wa 3, jambo ambalo upinzani unasema ni kinyume na katiba ya Burundi na makubalinao ya amani ya Arusha. 

Hata hivyo chama tawala cha CNDD-FDD kinaona kwamba rais Nkurunziza bado ana nafasi ya kuwania kutokana na muhula wa kwanza kuelezwa kwamba hakuchaguliwa na wananchi bali aliteuliwa kupitia bunge.

Patrick Spirlet amesema kumekuwa na maoni tofauti kuhusu muhula huu wa 3, hivyo wametaka maoni hayo yasikilizwe wakati huu tayari kanisa katoliki na Mashirika ya kiraia yameonyesha kupinga hatuwa hiyo ambayo hata hivyo Nkurunziza hajatangaza bayana kwamba atawania muhula mwingine.

Jumuiya ya kimataifa inatiwa wasiwasi na hali ya kisiasa nchini Burundi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, lakini hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Umoja wa Ulaya kuonyesha msimamo wake kuhusu muhula wa 3 wa rais Nkurunziza.

Patrick Spirlet amesema amani nchini Burundi bado ni legelege hivyo inabidi kuheshimu katiba ya nchi hiyo na kuheshimu pia mkataba wa amani wa Arusha uliofikia kusitishwa kwa vita mwaka 1993-2006

Akijibu hoja hii ya Umoja wa Ulaya waziri wa mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure amesema mkataba wa Arusha sio bibilia ambayo haiwezi kubadilishwa.

mardi 3 mars 2015

WIZARA YA SHERIA NCHINI BURUNDI YASEMA HUSSEIN RAJABU HAJATEKWA BALI AMETOROKA


Wizara ya sheria nchini Burundi imesema kwamba Hussein Radjabu kinara zamani wa chama tawala cha CNDD-FDD hakutekwa bali ametoroka jela kuu la mpimba na kutokomea katika maeneo yasiojulikana bado.

Kulingana na naibi msemaji wa wizara hiyo Bigirimana Eliason amesema Hussein Radjabu ametoroka katika jela kuu la Mpimba katika Usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu March 2 mwaka 2015 akiwa na wafungwa wengine 4, pamoja na askari polisi watatu

Naibu mseji huyo ameeleza kuwa mbali na Hussein Radjabu mfungwa mwingine Ribakare Baudoin maharufu Ndindi, Ndikuma Remy aliekuwa anahusika na Ulinzi wake na Irankunda Sirique liaekuwa mpishi pamoja na polisi watatu.

Hayo yanajiri wakati huu wakili wa Hussein Radjabu Prosper Niyoyankana akitishia kufunguwa mashtaka kutokana na mteja wake huyo ambae haijulikani alipo. Wakili huyo amesema mteja wake amekuwa akifanyiwa madhila na vitisho vya kuuawa alipokua jela.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...