Pages

mercredi 24 décembre 2014

MAHAKAMA YA KENYA YAKATAA KUSITISHA SHERIA KUHUSU USALAMA


mahakama kuu jijini nairobi hapo jana imetupilia mbali ombi la muunganbo wa upinzani nchini humo kutaka kutoa amri ya kusitisha utekelezwaji wa sheria tata zihusuzo usalama.

Muungano wa upinzani nchini Kenya Cord hapo jana ulikuwa umeitaka mahakama nchini humo kufuta sheria mpya iliodhinishwa na bunge hivi karibuni kuhusu usalama, sheria ambayo wakili wa upinzani James Orengo amesema ipo kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Mbali na kuwa kinyume na katiba ya nchi hiyo wakili huyo amesema imeidhinishwa katika mazingira tatanishi bungeni na kuitaka mahakama kusitisha utekelezwaji wa sheria hiyo kabla ya kutathminiwa upya.

Jaji mkuu wa mahakama Isaac Lenaola ametupilia mbali ombi hilo la upinzani na kudai kuwa umauzi wa kusitisha utelekezwaji wa sheria hiyo utakuwa kinyume cha sheria kutokana na upinzani kukosa sababu maalum za kuifanya mahakama kusitisha sheria hiyo.


jeudi 18 décembre 2014

BURUNDI, TUME HURU YA UCHAGUZI KULIKONI?

Tume ya Uchaguzi nchini Burundi CENI imekiri dhahiri shahiri kuwepo kwa kasoro zilizojitokeza wakati wa zoezi la kuorodhesha raia kwenye daftari la wapiga kura na kusisitIza kwamba ukiukwaji huo wa taratibu hautokani na uamuzi wa dhati wa Tume hiyo.

Mapema juma hili, vyama vya upinzani nchini humo vimeiomba tume hiyo kujiuzulu ambapo vyama 18 vimeituhumu Tume hiyo kuandika majina ya wapigakura hewa kusaidia chama tawala katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Vyama hivyo 18 vya upinzani nchini humo vinatishia kuendesha maandamano iwapo madai yao hayatopatiwa jawabu. Vyama hivyo vinaiomba tume ya uchaguzi Ceni pawepo na mazungumzo kuhusu matokeo ya zoezi la kuorodhesha raia wataopiga kura hapo mwakani na pia tume ya uchaguzi Ceni ijiuzulu kwa kuwa si huru.

Kumekuwa na hofu ya kutokea mvutano wa kisiasa nchini Burundi kutokana na hali hii ambayo tume ya Uchaguzi imeendelea kupuuzia madai ya wansiasa wa upinzani, jambo ambalo linaweza kukwamisha mchakato mzima wa uchaguzi kama ilivyoshuhudiwa katika chaguzi zilizopita.

Mbali na ukimya wa wa tume huru ambayo licha ya kukiri kuwepo na dosari imeendelea kusisitiza kwamba kasoro zilizojitokeza zinaweza kurekebishwa, rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza pia alitakiwa kuingilia kati kuhusu swala hili ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unashirikisha pande zote, ili baadae ataeangukia pua kwenye uchaguzi akose sababu.

Upinzani wao unaona kuwa kukaa kimya kwa viongozi wa chama tawala ni kutokana na jambo hili kukinufaisha.

Lakini pia Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, mashirika mbalimbali ya kimataifa yameendelea kukaa kimya kutokana na tuhuma hizi za uwepo wa udanganyifu katika zoezi hili la kuwaorodhesha wananchi katika dafatari la wapiga kura.

Kama kweli tume huru yenyewe inakiri uwepo wa kasoro nyingi tu katika zoezi hilo, kwanini madai ya upinzani yasifanyiwe kazi? Mwenyekiti wa tume hiyo CENI Pierre Claver Ndayicariye alisikika akisema kwamba chaguzi zilizopita kulikuwepo na dosari kama hizo, lakini zilirekebishwa, hivi hali ilivyokuwa kipindi hicho ndivyo ilivyo kwa sasa?

Wachambuzi wa siasa wanajiuliza wapo wapi watetezi wa Burundi? Wanasubiri moto uwake ili waje kuuzima wakati kuna uwezekano mkubwa wa kuuzima kabisa usiwake?

Kwa vyovyote vile hakuna ataefaidi iwapo vurugu zitatokea ikiwa chanzo itakuwa na swala hili ambalo baadhi wanalichukulia kuwa la kawaida wakati wengine walichukulia kuwa la msingi.

Tusubiri tuone.

UMOJA WA MATAIFA KUCHUNGUZA KUHUSU TUHUMA DHIDI JENERALI JEAN BOSCO KAZURA

Umoja wa Mataifa umeanza kufikiria na kujadili tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Mkuu wa majeshi ya Umoja huo ya kulinda amani nchini Mali - MINUSMA- Jenerali Jean Bosco Kazura kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita nchini Rwanda.


Mwezi Desemba mwaka 2013, mwandishi wa habari wa Canada Judi Rever alimtuhumu jenerali Kazura kutekeleza vitendo vya wa uhalifu wa kivita nchini Rwanda mwaka 1994 akiwa afisa mwandamizi wa Rwanda Patriotic Army Rwanda cha rais Paul Kagame.


Tangu tuhuma hizo zitolewe mwaka uliopita, Umoja wa Mataifa umekaa kimya lakini ple Jenerali Kazura ajiuzulu ukimya huo umeanza kuvunjwa na tuhuma kujadiliwa kwenye Idara ya Oparesheni za Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa.

mercredi 17 décembre 2014

MBIVU NA MBICHI HAPO KESHO BUNGENI NCHINI KENYA

Wabunge nchini Kenya hapo kesho alhamisi wanatarajiwa kuyapigia kura mapendekezo mapya ya sheria kuhusu usalama, mapendekezo ambayo serikali ya nchi hiyo inasema yatasaidia kupambana na maswala ya Ugaidi.

Hata hivyo mapendekezo hayo yanapingwa vikali na upinzani ambao umesema unataka yabadilishwe la sivyo watapiga kura ya hapana.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kuwazuia washukiwa wa Ugaidi kwa kipindi kirefu bila kupelekwa mahakamani, wanahabari kupata idhini ya polisi kabla ya kuchapisha picha au habari kuhusu Ugaidi.

Mbali na wabunge wa Upinzani wanahabari pia nchini humo wanapinga mapendekezo hayo na kutaka yabadilishwe.

Hivi karibuni rais wa nchi Uhuru Kenyatta alisikika akisikitishwa na mvutano wa wabunge kuhusu swala la Usalama, ambapo waheshimiwa hao walifikia hatuwa ya kuvutana mashati.

BAN KI MOON KUZURU NCHI ZA AFRIKA MAGHARIBI HIVI KARIBUNI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon anataraji kuzuru hivi karibuni katika nchi nne za ukanda wa Afrika Magharibi zilizo athiriwa na mlipuko wa Ebola. Ziara hii inakuja wakati nchi ya Sierra Leone ikiongeza muda wa kampeni ya nyumba kwa nyumba kuhusu Ebola.
Kulingana na duru za kidiplomasia kutoka Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon atatembelea nchini Liberia, Guinea, Sierra Leone na Mali katika tarehe mbayo haijatajwa.
Ebola ambayo ilianza kuzungumziwa kusini mwa Guinea mwezi Desemba mwaka jana, tayari imegharimu maisha ya watu 6.900 dhidi ya jumla ya watu watu 18.500 waliodaiwa kuambikizwa virusi ikiwa ni sawa na asilimia 99 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea ikiwa ni takwimu za hivi karibuni za shirika la Afya duniani WHO.
Nchini Mali ambako watu saba wameripotiwa kiupoteza maisha kutokana na Ebola, hali hali bado ni tete licha ya kuondolewa kwa hali ya uchunguzi dhidi ya watu wanakisiwa kuwa karibu na wahanga wa Ebola kukutwa hawana virusi hivyo
hayo yanajiri wakati viongozi wa Sierra Leone wakitangaza kuongeza muda wa kampeni ya nyumba kwa nyumba juu ya kuhamasisha kuhusu virusi vya Ebola ambapo kampeni hiyo iliobatizwa "Western Area Surge" itaendelea hadi Desemba 31.


RAIS WA TCHAD AYATUHUMU MATAIFA YA MAGHARIBI KUZUA UGAIDI KWA KUMUUWA GADAFI NCHINI LIBYA

Baada ya mazungumzo ya siku mbili jijini Dakar, katika jukwa la kwanza la kimataifa kufanyika juu ya Amani na Usalama barani Afrika jukwa ambalo liliandaliwa kwa ushirikiano na diplomasia ya Ufaransa, jambo ambalo halijapokelewa vizuri na Umoja wa Afrika AU.

Licha ya wajumbe wote walioshiriki katika mkutano huo kuridhishwa na mazungumzo, swala la Ugaidi nchini Libya limeonekana kugusa hisia za viongozi wengi mkutanaoni na kuzua mjadala mkali kuhusu jukumu la majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi Nato katika kuuangusha utawala wa hayati kanali Muamar Gadafi


Rais wa TChad Idriss Deby Itno amesisitiza kuwa Lengo kuu la majeshi ya Nato nchini Libya ilikuwa ni kutekeleza mauaji ya rais Gaddafi na si vinginevyo na kwa hiyo NATO pamoja na Umoja wa Mataifa vinatakiwa kuwajibika kurejesha amani nchini Libya. 

URUSI YASEMA TUNAUWEZO WAKUKIDHI MAHITAJI YETU

Waziri mkuu wa Urusi Dimitri Medvedev amesema kwamba Urusi inauwezo wa kutosha kutatua matatizo yake ya kifedha ilionayo kwa sasa yatokana na kuanguka kwa sarafu yake ya Ruble bila hata hivyo kudhoofisha kanuni za uchumi wa soko.

Medvedev amesisitiza kwamba nchi yake ina rasili mali za kifedha ambazo zinaweza kuisaidia serikali kufikia malengo yake ya kiuchumi na Pia ina bidhaa zinazo hitajika ili kuhakikisha mahitaji yanakwenda sambamba

Waziri mkuu huyo ameyasema hayo katika mkutano wa dharura kwenye runinga ya taifa na mawaziri wake kutoka katika sekta ya uchumi na wawakilishi ma wamakapuni yanayo safirisha bidhaa kwenda nje ya nchi hiyo na kutupilkia mbali kanuni iliozidi uhusuyo soko.

ANGALIA PICHA ZA WASANII WATAOSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA IKOH EVENT BUJUMBURA

Hii sio ya kukosa kabisa,  moja miongoni mwa tamasha kubwa la mwisho wa mwaka jijini Bujumbura. Hakuna caption ndefu picha zenyewe zinajitosheleza.

















KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...