Pages

lundi 14 décembre 2015

MAREKANI YAWATAKA RAIA WAKE KUONDOKA BURUNDI

Serikali ya Marekani imewataka raia wake wanaoeshi nchini Burundi kuondoka mara moja nchini humo kufuatia kuendelea kuhatarishwa kwa hali ya usalama nchini humo tangu pale lilipofeli jaribio la mapinduzi mwezi Mei mwaka huu lililofuatiwa na machafuko na mzozo wa kisiasa.

Katika taarifa ya wizara ya mambo ya nje wa Marekani hapo jana imewataka raia wa Marekani wasiokuwa na shughuli muhimu kuondoka nchini humo na familia zao na kuwataka raia wote wa Marekani kutoelekea Burundi, na wale waliopo nchini humo kuondoka haraka iwezekanavyo.

Zaidi ya watu 90 wameuawa siku ya Ijumaa Juma lililopita baada ya kutokea kwa mashambulizi ya kambi tatu za kijeshi nchini humo, ambapo taarifa za jeshi la nchi hiyo ziliarugu kuuawa kwa waasi 79 na wanajeshi 8.

Jumamosi asubuhi maiti kadhaa zilizshuhudiwa katika mitaa ilioendesha maandamao ya kupinga muhula wa 3, ambapo wengi wa waliouwawa ni vijana. Mashuhuda nchini humo wamevituhumu vikosi vya Usalama kuwashikilia vijana waliokutana nao baada ya shambulio la kambi za kijeshi na kuwauwa, ambapo maiti kadhaa zilionekana zikifungwa kamba mikononi.

Kulingana na taarifa ya pamoja ua mjumbe wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini na kamishna wa ushirikiano wa kimataifa Neven Mimica wameomba ukweli uwekwe wazi kuhusu mauaji haya yanayotokea katika karne hii.


vendredi 11 décembre 2015

HALI YA SINTOFAHAM YAENDELEA KURIPOTIWA NCHINI BURUNDI BAADA YA KUTOKEA SHAMBULIO LA KAMBI YA KIJESHI









Hali ya sintofahamu yaebdelea kushuhudiwa jijini Bujumbura ambapo vyombo vya usalama vimezingira maeneo kadhaa ya jiji la Bujumbura.

kwa Mujibu wa msemaji wa jeshi Kanali Gaspard Baratuza, Kundi la watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito, wametekeleza mashambulizi mfululizo katika kambi mbili za jeshi jijini Bujumbura, Burundi, ambapo wapiganaji 12 wameuawa na wengine zaidi ya 24 wametiwa mbaroni, huku wanajeshi wa serikali wanaokadiriwa kufikia watano nao wakiuawa wakati wa makabiliano.

Mashambulizi haya yakupangwa, ni mabaya zaidi kutekelezwa toka kulipofanyika jaribio la mapinduzi lililoshindikana mwezi May mwaka huu.

Wapiganaji hao walivamia kambi ya jeshi ya Nagara kaskazini mwa mji wa Bujumbura pamoja na kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Iscam, kilichoko kusini mwa nchi hiyo, baada ya kupora silaha katika kambi moja eneo hilo mashambulizi yaliyoanzwa kutekelezwa alfajiri ya hii leo na kudumu kwa zaidi ya saa nne

Kuliripotiwa pia makabiliano ya risasi katika viunga kadhaa vya jiji la Bujumbura, hali inayozidisha hofu ya kiusalama kwenye taifa hilo, wakati huu ambapo inadaiwa kuwa rais Pierre Nkurunziza amefanya kikao cha dharura na mawaziri wake kuizungumzia hali hiyo.

Shughuli zimesimama jijini Bujumbura, hakuna mawasiliano ya watu kutoka katika mtaa mmoja kuelekea mtaa mwingine, hali ambayo inalalamikwa na wananchi wa kaazi wa jiji la Bujumbura baada ya kukosa chakula kutokana na kuzuiliwa kwa barabara zote kuu

Polisi na wanajeshi nchini Burundi, wanasema wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hili pamoja na kuendesha msako wa wapiganaji zaidi walioripotiwa kukimbia baada ya mashambulizi haya.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mashambulizi ya hivi leo, lakini Serikali inasisitiza kuwa ni makundi ya waasi wanaotaka kuipindua Serikali.

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...