Watu
wawili wanaodaiwa kuwa huenda walikuwa wamebeba mabomu wameuawa kwa
kupigwa risasi, na polisi mmoja kujeruhiwa nje ya ukumbi ambao
kulikuwa kunafanyika mashindano ya kuchora kikaragosi cha Mtume
Muhammed mjini Texas, Marekani.
Kwa
mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo kutoka taasisi ya Marekani ya
kulinda uhuru wa kutoa maoni, wamesema kuwa watu hao waliuawa baada
ya kurusha risasi kuelekea sehemu ambayo shindano hilo lilikuwa
linafanyika na ndipo polisi walipolazimika kutumia nguvu kuwakabili.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hili, wanasema kuwa wakati shindano hilo
likiendelea, watu wawili waliokuwa na silaha na vifaa vinavyodaiwa
kuwa ni mabomu walianza kusogea kwenye eneo la tukio na kabla ya
kufika waliwafyatulia risasi polisi walipkuwa jirani na kuwalenga
baadhi ya watu waliohudhuria kabla ya kuuawa na kikosi maalumu cha
Polisi wanajeshi.
Polisi
mjini Texas wanasema wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini sababu
iliyowafanya watuhumiwa hao kuwafyatulia risasi waandaaji wa shindano
hilo, ingawa baadhi ya watu wamewakosoa watu walioandaa shindano hilo
wakijua fika kuwa lazima lingewakera baadhi ya waumini wa dini ya
kiislamu.
Waumini
wa dini ya kiislamu wamelaani shambulio hili lakini wakawakosoa
waandaaji wa shindano hilo ambalo mshindi alizawadia dola za Marekani
elfu 10 kwa kuchora kibonzo wa kinachomuonesha Mtume Muhammad.
Tukio
hili linajiri ikiwa ni miezo michache tu imepita toka kushambuliwa
kwa ofisi za gazeti la Charlie Hebdo nchini Ufaransa ambalo
lilichapisha kibonzo cha mtume Muhammed, ambapo watu wenye silha
waliwashambulia wafanyakazi wake na kuua watu 16.