Hatimae
wapigambizi nchini Indonesia wamefaulu kukipata kisanduku cha ndege
ya Malesia AirAsia ilioanguka katika bahari ya Java Desemba 28
iliopita ikiwa na habiria 162 ikiw an hatuwa muhimu katika juhudi za
kutafuta mabaki ya ndege hiyo.
baada
ya takriban majuma mawili ya shughuli za uokozi Mkurgenzi wa idara ya
uokozi Bambang Soelistyo, hatimae kisanduku kinacho rikodi sauti
cha ndege iliokuwa ikiunganisha Indonesia na Surabaya nchini
Singapour kimepatikana na sasa wanajaribu kutafuta kifaa maalum
kinachorikidi sauti ili kufaham zaidi kuhusu mawasiliano ya mwisho ya
rubani wa ndege hiyo.
Kiongozi
wa jeshi jenerali Moeldoko amesema kuna matumaini ya kupata
kisanduku kingine na kifaa kinacho rikodi sauti hakiko mbali sana na
eneo hilo. Jenerali huyo amesema matumaini haya yanakuja baada ya
kuwepo kwa viashiria katika eneo hilo.
Mtaalamu
mmoja wa kamati ya kitaifa ya usalama wa usafiri kimataifa Mardjono
Siswosuwarno amesisitzz kwamba kisanduki hicho cheusi kilichopatikana
kitasafirishwa hadi jijini Jakarta kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Ndege
hiyo ya kampuni ya Malesia ilianguka desemba 28 muda mfupi baada ya
kupaa angani eneo la Surabaya wakati ikielekea nchini Singapour.
Viongozi
wa indonesia wanasema rubani wa ndege hiyo iliokuwa na habiri zaidi
ya mia moja aliomba ruhusa ya kupaa juu zaidi kuepuka mawingi
yaliokuwa tishio, lakini hakuweza kupjibiwa kutokana na mawasiliano
kuwa mengi katika sekta hiyo, ambapo mawasiliano kati ya ndeger hiyo
na idara ya uchunguzi yalitoweka muda mfupi baadae.